Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Klabu ya Newcastle wamemfukuza kocha Steve Bruce baada ya tetesi za muda mrefu kabla ya timu hiyokuchapwa na Tottenham Hotspurs Jumapili.

Tetesi zinasema, Chelsea wako tayari kumfanya kiungo wa England Mason Mount kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa zaidi wakati klabu hiyo ikijiandaa kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na nyota huyo mwenye miaka 22.

Mshambuliaji wa Hispania Ansu Fati, 18, anakaribia kusaini mkataba mpya wa muda mrefu kusalia Barcelona kukiwa na kipengele cha ada ya £846m akitaka kuondoka kama ikivyo kwa Pedri, 18.

 

Beki wa kulia wa Atletico Madrid na England Kieran Trippier, 31, ambaye alikua akihusishwa sana na mipango ya kuhamia Manchester United katika majira ya joto, anasema angelipenda kucheza ligi kuu ya England kwa mara nyingine.

Tetesi zinasema, Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer ana mpango wa kuwaondoa angalau wachezaji watano dirisha la Januari likifunguliwa.

Tetesi zinasema, Klabu za Liverpool, Borussia Dortmund au RB Leipzig zitapaswa kulipa kati ya 30m na 40m euros kupata saini ya mshambuliaji wa RB Salzburg na Ujerumani Karim Adeyemi, 19.

Mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 22, hana furaha pale Juventus, hali inayomsukuma wakala wake Mino Raiola kufanya mazungumzo na Barcelona kuhusu uwezekano wa kuhamia huko.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Aston Villa itapaswa kuharakisha kumsaini nyota wa River Plate Julian Alvarez kwakuwa klabu ya ligi kuu Italia (Serie A) ya AC Milan wanamtaka pia mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 21.

Klabu za Newcastle United, Leeds United zitamkosa kiungo wa Blackburn Rovers muingereza Joe Rothwell baada ya nyota huyo mwenye miaka 26 kuamua kusaini klabu ya Rangers.

West Ham United wanamfuatilia mlinda mlango wa Barcelona Neto, 32, ambaye atakua tayari kusaini mkata wa mkopo na kuondoka Nou Camp mwezi Januari iwapo klabu itakayomsajili itakubali kumsajili mbrazil huyo moja kwa moja katika dirisha kubwa la usajili la majira ya joto.


KUSANYA MKWANJA NA BIG BAD WOLF

Mchezo wa Big Bad Wolf ni moja ya michezo pendwa katika kasino zetu za meridianbet. Ukiachana na tabasamu utakalolipata wakati wa kucheza pia unajiwekea nafasi ya kuwa mshindi wa mkwanja mrefu unaotoka kila baada ya mzunguko kukamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.