Lendari wa Urusi wa MMA, veterani Fedor Emelianenko amemchimba biti bondia Conor McGregor kuwa anatakiwa ‘achunge domo lake’. McGregor anafahamika sana kwa kuropoka ropoka au kuongea ‘mbofu mbofu’ juu ya wapinzani wake na baadhi ya watu anaoamua kuwadisi.
Veterani huyu wa ngumi za uzani mkubwa -Heavyweight ameona si sawa asipomtupia neno jamaa ili apunguze kupiga domo. Emelianenko anajiandaa kwa ajili ya pambano lake ambalo linaweza kuwa la mwisho dhidi ya mmarekani Ryan Bader kwenye fainali Bellator Grand Prix kule Calfonia wikiendi hii.
Bingwa huyu anafahamika pia kwa jina la The Last Emperor, ni moja kati ya watabe wanaogopwa sana kuingia ulingoni. Katika maandalizi yake kuelekea pambano lake amewachana wote ambao wanatabia ya kuongea shombo dhidi ya wenzao akimtaja pia McGregor.
Jamaa ametuma ujumbe wake pia kwa Mapromota kuwa hakuna haja ya kuvumilia watu wanaotukana sana kama ambavyo McGror alifanya kwa Nurmagomedov, lakini pia anadhan Nurmagomedov hakupaswa kuchukua hatua alizochukua baada ya kusemwa vibaya na McGregor.


Issa
Emiliano mc gregory atakugalagaza tu