Gareth Bale amekuwa mchezaji wapili kwenye timu ya taifa ya Wales kuweza kufikisha michezo 100 ya kimataifa baada ya Chris Gunter.
Gareth Bale hakuonekana kwa takribani kipindi cha miezi miwili kutokana na meajeruhi, lakini alionekana kujihamini usiku wa jana na kuiaidia timu yake ya taifa kuweza kuibuka na ushindi wa kishindo dhid ya Belarus.
Bale alifanyiwa mapokezi ya aina yake kwenye dimba la Cardiff City Stadium huku akipewa heshima kama jenerali wa vita aliye rudi nyumbani na ushindi, wakati dakika 45 tu zilitosha kumuwezesha Bale kuingia kwenye kumbukumbu za Wales.
Gareth Bale amebakisha michezo saba tu kuweza kuipiku kumbukumbu iliyowekwa na Chris Gunter ya kuwa mchezaji aliyeichezea timu ya taifa ya Wales michezo mingi zaidi ya kimataifa.
Ushindi wa jana wa Wales unawapeleka mpaka nafasi ya pili nyuma ya Belgium kwenye kufuzu kombe la Dunia nchini Qatar wakiwa na utofauti wa pointi tano.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?



