Kiungo wa Monaco Aurelien Tchouameni anavivutia vilabu mbalimbali barani Ulaya baada ya kuonyesha kiwango bora nadni ya Ligue 1 pamoja na kufanikiwa kuitwa katika timu ya taifa ya Ufaransa.
Klabu ya Real Madrid ni miongoni mwa vilabu vilivyoonyesha nia ya kutaka kupta huduma ya mchezaji huyo wa miaka 21 lakini siyo wao pekee yao waliona kipaji cha kiungo huyo bali Chelsea pia wanamtolea macho Tchouamen na wamemuweka katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa kutua darajani.
Na klabu hiyo ya Premier League ndio wagombea wakuu na wanatarajia mchezaji huyo wa Monaco kuhamia The Blues majira ya joto yanayokuja.
Kwa mujibu wa Transfermarkt, kinda huyo anaweza kupanda thamani kutoka euro milioni 18 mpaka euro milioni 36 tangu kuanza kwa msimu huu.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


