Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Kenya ashikiliwa na jeshi la polisi kwa kashfa za rushwa na atakaa lumande kwa siku 14 kupisha uchunguzi wa mashtaka hayo.
Leo jumatatu mahakama ya nchini Kenya ilitoa kibali cha kuwaruhusu polisi kumshikillia Nick Mwendwa, raisi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Kenya (FKF) kwa siku kumi na nne kupisha uchunguzi wa mashtaka ya rushwa.

Mwenda alikamatwa siku ya ijumaa baada ya waziri wa michezo Amina Mohamed, kutangaza kusambaratika kwa shirikisho hilo baada ya serikali kufanya uchunguzi na kukuta kuna ubadhirifu wa pesa ambazo serikali ilizota na wadhamini wengine.
Mwenda mwenye miaka 41 amekuwa raisi wa shirikisho hilo tokea mwaka 2016 na amevuliwa madaraka hayo mpaka atakaposibitishwa kuwa hana hatia, na kwa sasa waziri ametangaza baraza ambalo litaongoza taasisi hiyo kwa muda wa miezi sita.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


