Paul Scholes Pengine Ndio Kiungo Bora Zaidi wa Muda Wote

Msururu wa viungo wote duniani aliovaana Paul Scholes yupo mmoja Zinedine Zidane alimzimia sigara, hadi leo anaamini hajawahi kukutana na kiungo mgumu zaidi yake.

Pengine ndiye mchezaji pekee anayejuta kutokucheza nae. Mpaka leo haamini kama alistaafu hajavaa jezi moja na Scholes. Kwa Zidane, Paul Scholes ndiye kiungo bora zaidi kwa kizazi chake.

Paul Scholes
Paul Scholes

Subiri kwanza! Namzungumzia Zidane aliyecheza na Patrice Vierra, Claude Makelele na Luis Figo. Kumbuka kipindi fulani alikuwa na Eric Cantona kwenye dimba la Ufaransa.

Ni Scholes huyu ambaye hata Xavi na pasi zake anakiri kwamba macho yake yalipenda kumtazama. Unajiita vipi kiungo wa mpira wakati hujifunzi kwa Paul Scholes??

Hata Sir Alex Ferguson na misimamo yake yote bado anakubali kwamba ana wachezaji wanne tu bora aliozawadia na Mungu! Wengine aliwatengeneza mwenyewe.

Paul Scholes
Paul Scholes

Katika kitabu chake cha Leading anasema, mikononi mwake walipita wachezaji wanne tu waliozaliwa na vipaji asilia, hawakuhitaji kutengenezwa. Cristiano Ronaldo, Eric Cantona, Ryan Giggs na wa nne malizia mwenyewe.

Katika safari zake zote vitani alikuwa na kamanda Paul Scholes wa kudhibiti askari wote wa miguu katikati ya kiwanja. Wakati huohuo aliliongoza jeshi lake la anga kule mbele.

Iwe ni usiku wa baridi kali la Ulaya kama ule wa Moscow dhidi ya Chelsea, au iwe ni weekend ya jasho na damu la ligi kuu katika uwanja korofi zaidi duniani Anfield, Scholes alikuwepo kuamrisha na kuongoza jeshi lake.

Nasema hivi nikiukumbuka ukabaji wake wa kikatili. Katika mazingira ya ‘hamsini kwa hamsini’ yeye angekupa thelathini halafu yeye achukue sabini. Hakuwa na fair competition kabisa😀

Ndiyo maana Arsene Wenger alikuwa anamlalamikia sana. Wenger anadai soka la Scholes lina giza sana ndani yake. Lakini ni unafiki tu! Si Wenger huyuhuyu alikuwa anampa mkono Vieirra baada ya kutegua watu mabega??

Hata mshambuliaji wake bora wa muda wote Thierry Henry anafahamu balaa lake. Henry anadai hakupenda kabisa kucheza mechi za Scholes. Hata hivyo huwezi kupenda mateso. Kucheza dhidi yake ni kupewa gereza ya dakika tisini.

Alisimama kwenye kiungo cha Manchester United kwa miaka 20. Leo ametimiza miaka 47.


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.