Nyota Eric Garcia amemfananisha meneja mpya wa Barcelona Xavi Hernandez na Pep Guardiola na Luis Enrique.
Eric Garcia amefanya kazi chini ya meneja Pep Guardiola akiwa Manchester City, ambao aliachana nao na kurejea Barcelona. Nyota huyu pia alifanya kazi na Luis Enrique kwenye timu ya taifa ya Hispania.

Xavi ameanza majukumu mwisho wa wiki iliyopita, lakini tayari joto la mabadiliko limeanza kuonekana Barcelona.

Kwa mujibu wa Garcia, Xavi ni mtu sahihi kuiongoza Barcelona kwa sasa.
“Ni mtu sahihi kuiongoza Barcelona. Kwa Xavi ninaona vitu kutoka kwa Pep (Guardiola) na Luis Enrique pia. Ni legendari wa timu na kocha mzuri.” – Garcia
Lakini pia Garcia alimzungumzia mtangulizi wa Xavi kuwa kwa upande wake alimsaidia katika vitu mbalimbali mpaka alipofikia sasa. Akimzungumzia Ronald Koeman alinukuliwa akisema
“Kwa upande wangu, alinisaidia sana na sina maneno zaidi ya kusema ahsante.” Garcia
Kibarua rasmi cha Xavi kinaanza pale kikosi chake kinapokutana na Espanyol jumamosi hii.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


