Simba Ingemvumilia Gomez tu, Kocha Mpya Ataweza?

Binafsi niseme tu Simba lazima wakubali kwamba sasa hivi ligi imebadilika na ligi ni ngumu haswaa maana ligi ina pesa sasa hivi wasitarajie wepesi maana kila timu unayokutana nayo sasa hivi inakaza

Sasa hivi timu za madaraja ya kati haziangalii tunaenda kucheza na Simb au Yanga, na zenyewe zinataka matokeo mazuri ili kujiweka pazuri mwishoni mwa msimu, haziitaji kufungwa kirahisi ndio maana unaona sasa hivi wanapata tabu

Simba

Kuondoka kwa Chama na Luis hakujafanya Simba ipunguze kasi yake! kwa kua tayari ilikua  inawachezaji wengi na ni wazuri kabisa, sema mashabiki na viongozi hawataki kukubaliana na hali iliyopo kwamba ligi inaushindani kwasasa huwezi kutawala miaka yote

Kwani walivyokuwepo hao wachezaji wawili waliouzwa Simba ilikuwa haifungwi? upepo umebadilika na Wana msimbazi wasipotulia na kutuliza vichwa watapotea sana

Msimbazi ilikuwa haihitaji kocha mpya yeyote kwa kipindi hiki, Gomez alikuwa kocha mzuri tu walitakiwa waendelee kufanya kazi na Suleiman Matola, na kwa Simba hii hata wangemuachia Matola ingefanya vizuri tu sema kocha Matola hakuwa na vigezo

Simba

Wana lunyasi memleta kocha mpya kwa sifa kibao na CV kubwa lakini CV yake haichezi mpira kwenye kiwanja cha mpira wa miguu! kikubwa kama kocha mpya kaja wawe na uvumilivu sio wanafungwa mechi moja mbili au wanatoka sare waanze kelele, yatakuwa ni yaleyale

Wamemfukuza Gomez na alikuwa kocha mzuri sana hakuwa na tatizo lolote, hata Hitimana na Matola wangeachwa tu Simba ingecheza mpira, kuna upepo umebadilika tu ndio maana hata kina Peter Banda unaona hawajaingia kwenye mfumo


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.