Mauro Icardi ameripotiwa kuwa katika kipindi fulani cha sintofahamu pale klabuni Inter Milan huku akivuliwa unahodha klabuni hapo. Baadhi ya tetesi ziliripoti kuwa suala hilo linahusiana na mipango yake ya kusepa klabuni hapo. Hata hivyo ripoti za hivi karibuni zaidi zinadai kuwa nyota huyu atabaki klabuni hapo licha ya kuvuliwa unahodha.
Nyota huyu wa miaka 25 alikuwa anahusushwa na vilanu vya Real Madrid, Manchester United na Barcelona licha ya mkataba wake kusiha mwaka 2021. Staa huyu hakuwepo kwenye kikosi dhidi ya Rapid Vienna gemu ya Europa League na pia hakuwepo kwenye kikosi kilichoshinda bao 2-1 dhidi ya Sampdoria.
Mke wa staa huyu, ambaye pia ni wakala wake amesema kuwa nyota huyu hana mpango wa kuondoka klabunoi hapo. Yeye kama wakala huwa anakuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na klabu hiyo, lakini anasisitiza kuwa mmewe ana mapenzi zidi na timu hiyo na mara zote byupo tayari kuchagua kuendelea kuivaa jezi ya klabu hiyo zaidi kuliko pesa nyingi.


Fatina mfingi
Makala nzur