Pierre-Emerick Aubameyang anaripotiwa kuwa windoni kwenye rada za vilabu vitano huku kukiwa na uvumi kuhusu hatma yake na Arsenal.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 ameshindwa kuonesha kiwango chake cha kawaida kwa miezi 12 iliyopita.
Mkataba wa sasa wa Pierre na Washika Bunduki unadumu hadi 2023, hii ni baada ya kuongeza mkataba wake msimu wa joto uliopita, lakini anaendelea kuhusishwa na kuondoka akionekana kushindwa kufanya vyema mbele ya nyavu.
Kwa mujibu wa Fichajes, Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid, Inter Milan na AC Milan zote ziko tayari kupambania saini ya Aubameyang mwaka 2022.

Ripoti hiyo inadai kwamba siku za staa huyu na Arsenal zinahesabika, na huenda akapewa tiketi ya kuondoka Januari mwakani huku Arsenal ikilenga kupokea ada kubwa kwenye biashara ya mshambuliaji huyo.
Aubameyang ana jumla ya mabao 92 katika michezo 162 akiwa na The Gunners kwa michuano yote lakini kwa sasa ameshindwa kuzitendea haki nyavu katika mechi tano mfululizo za Ligi Kuu ya Uingereza.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


