Amadou Haidara Atakuwa Usajili wa Kwanza wa Ralf Rangnick?

Kiungo wa RB Leipzig Amadou Haidara anatajwa kuwa atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Manchester United chini ya meneja Ralf Rangnick.

Mashetani Wekundu watakuwa chini ya ulezi wa muda wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 63 kwa mara ya kwanza Jumapili hii kwenye gemu ya Ligi Kuu dhidi ya Crystal Palace.

Rangnick amekiri kwamba uhamisho wa Januari utakuwa mgumu kwa klabu, lakini Haidara anafikiriwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaolengwa zaidi na Mjerumani huyo kwenye dirisha la uhamisho la majira ya baridi.

Amadou Haidara Atauwa Usajili wa Kwanza wa Ralf Rangnick?
Amadou Haidara

The Sun wameripoti kwamba United wanajiandaa kutumia kipengele chake cha kuachiliwa cha pauni milioni 32 mwezi ujao huku Rangnick akikaribia kusajili mchezaji wake wa kwanza wa Red Devils.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa Rangnick amekubali dili la mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kufuatia mazungumzo na wakala wake, na ushiriki wake katika Kombe la Mataifa ya Afrika na Mali hautaleta changamoto.

Haidara anajivunia mabao 10 na asisti sita katika mechi 100 akiwa na Leipzig katika mashindano yote, na mkataba wake na timu hiyo ya Bundesliga unaisha mwaka 2025.


 

MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe