Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Manchester City na England Phil Foden, 21, ana thamani ya £128m na ni miongoni mwa wachezaji ghali zaidi duniani.

Real Madrid wana matumaini kwamba beki wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger , 28 ataweka mkataba wa mapema na klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari na kujiunga nao katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao.

Tetesi zinasema, Chelsea inalenga kumsajili kiungo wa kati wa Brazil na Real Madrid Casemiro, 29.

 

 

Tetesi zinasema, Ombi la West Ham la kutaka kumsajili mchaezaji wa Ulbegiji Eden Hazard kwa dau la £21m limekataliwa na Real Madrid.

Liverpool inawanyatia winga wa Leeds na Brazil Raphinha, 24, na mshambuliaji wa West Ham Jarrod Bowen, 24, kabla ya kuwasajili katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

Tetesi zinasema, Liverpool pia inamfwatilia mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 28.

Mkufunzi wa Barcelona Xavi anatarajiwa kuamua kuhusu usajili wa mwezi Januari wa kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong, 24, Beki wa Marekani Sergino Dest, 21, na kipa wa Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 29.

 

Coutinho Awekwa Sokoni na Barcelona.

Tetesi zinasema, Barcelona pia huenda ikamuuza kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 29, na beki wa Ufaransa Samuel Umtiti, 28.

Borussia Dortmund wanapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Red Bull Salzburg na Ujerumani Karim Adeyemi,19, ambaye pia anahusishwa na klabu ya Bayern Munich na Liverpool.

Paris St-Germain inataka kuwauza wachezaji mwezi januari , akiwemo mshambuliaji Mauro Icardi, 28, kiungo wa kati wa Brazil Rafinha, 28, na beki wa kati wa Senegal Abdou Diallo, 25.


AGENT JANE BLONDE AMEREJEA MSIMU WA SIKUKUU.

Unaweza kujishindia mamilioni katika kasino yako pendwa ya meridianbettz, mchezo wa Agent Jane Blonde Return ni moja ya michezo inayopendwa kwasasa huku ikiwafanya wachezaji kuwa mamilionea kila siku. Unasubiri nini! ungana na Agent Jane Blonde akufanye milionea.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.