Eddie Nketiah Bado Anapania Kuwakacha Arsenal

Eddie Nketiah anaripotiwa kuwa bado yupo tayari kuondoka Arsenal wakati wa dirisha la usajili la Januari.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga hat-trick mapema wiki hii huku The Gunners wakiandikisha ushindi wa 5-1 dhidi ya Sunderland katika mechi ya robo fainali ya Kombe la EFL.

Hata hivyo, mhitimu huyo wa akademi amecheza kwa dakika 38 pekee za soka la Premier League msimu huu, ikiwa ni sababu yake ya msingi ya kukataa mkataba mpya klabuni hapo.

Eddie Nketiah Bado Anapania Kuwakacha Arsenal
Eddie Nketiah

Licha ya Mikel Arteta kusema mara kwa mara kwamba anataka huduma za fowadi huyo, gazeti la Daily Mail linasema kwamba kwenye soko la Januari mambo yanaweza kubadilika.

Pamoja na kuweza kusaini mkataba wa awali wa kandarasi na klabu ya kigeni, Nketiah anavutiwa na timu nyingine za ligi kuu ya Uingereza, zikiwemo West Ham United, Crystal Palace na Brighton & Hove Albion.

Uamuzi wa kumuuza Nketiah yanategemea ikiwa Arteta atasuluhisha hali yake inayoendelea na Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka kwenye Uwanja wa Emirates kutokana na utovu wake wa nidhamu wa hivi punde.


KUWA BINGWA MSIMU HUU WA SIKUKUU NA OCEAN CALL

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.