Manchester United wameripotiwa kumtambua Mauro Icardi wa Paris Saint-Germain kama mbadala wa Edinson Cavani kwenye dirisha la usajili la Januari.
Cavani anaaminika kutaka kuondoka kwa Mashetani Wekundu mwanzoni mwa 2022, huku Barcelona wakiibuka kuongoza mbio za kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay, ambaye mkataba wake unamalizika Old Trafford Juni ijayo.
Kwa mujibu wa Calciomercato, Man United tayari wanajiandaa kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji huyo na wanamwona Icardi kama mchezaji anayefaa kuchukua nafasi ya cavani.

Hata hivyo, United wanatajwa na vyanzo kadhaa kuwa huenda wasifanye manunuzi yoyote kwenye soko la Januari wakijaribu kupunguza ukubwa wa kikosi chao.
Lakini ripoti ya Calciomercato inadai kuwa Juventus pia wanatamani sana kumnunua Icardi mwezi Januari.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye pia anahusishwa na Chelsea na Arsenal, ametikisa nyavu mara tano katika mechi 20 akiwa na PSG wakati wa kampeni za 2021-22.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

