Anajulikana kwa kusema kile anachokiamini bila kupindisha maneno. Rio Ferdinand, beki kisiki kwenye historia ya Manchester United.
Ferdinand aliitumikia United kati ya mwaka 2002-2014 akitua Old Trafford akitokea Leeds United. Wakati ule, Rio Ferdinand alicheka kama beki wa kati akishirikiana kwa karibu na Nemanja Vidic, kwa pamoja, walitengeneza ukuta mgumu zaidi kwenye historia ya EPL.

United ya miaka ile, sio United ya sasa. Kwa msimu huu pekee, The Red Devils wamesharuhusu nyavu zao kutikiswa mara 26 ikiwa ni mara mbili zaidi ya idadi ya magoli waliyofungwa Man City ambao ni vinara wa EPL mpaka sasa.
Rio Ferdinand amejipigia pande kurudi Old Trafford. Kwa mujibu wa Rio, endapo United watamuhitaji kama kocha wa idara ya ulinzi, hatosita wala kujifikiria mara mbili, yupo tayari. Hii itawezekana endapo tu, United wataonesha nia ya kumuhitaji.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

