Wakati wakipambana kuokoa jahazi lisizame msimu huu, Newcastle United wanampango wa kuingia mazima kwa Kieran Trippier kwenye usajili mdogo.
Dirisha dogo la usajili limefunguliwa rasmi leo nchini Uingereza, Scotland, Ujerumani na Italia. Vilabu vitakuwa na mwezi mmoja kufanya maboresho ya vikosi vyake ndani ya mwezi Januari, 2022.
Hili ni dirisha la usajili la kwanza kwa wamiliki wapya wa Newcastle United wakiwa na kocha mpya, Eddie Howe. Wakiwa wameshinda mchezo 1 pekee mpaka sasa kwenye EPL, hii ni fursa kwa The Magpies kuweka sawa kikosi chao katika harakati za kujinasua kutoka kwenye nafasi za kushuka daraja.

Kieran Trippier anatajwa kuwa mchezaji namba 1 anayehitajika zaidi pale St. James’ Park kwenye dirisha hili la usajili. Trippier amebakiza muda mfupi kabla mkataba wake na Atletico Madrid kumalizika. Hii ni fursa kwa Trippier kurejea Uingereza kama anavyotamani. Kwa Atletico, hii ni fursa ya kupata pesa kidogo kwenye usajili huu endapo Newcastle watapeka ofa kamili.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

