Tetesi zinasema, Tottenham wanataka kusajili mchezaji wa Barcelona na Brazil, Philippe Coutinho, 29 kwa uhamisho huru, Barca wanataka pauni milioni 17 kumuachia.
Tetesi zinasema, Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 16.8 zinazohitajika kumsajili mshambuliaji wa River Plate, Julian Alvarez, 21 mwezi Januari.
Newcastle wanakaribia kufikia makubaliano na beki wa Atletico Madrid, Kieran Trippier, 31, huku kukiwa na vipengele vinavyohusu kushuka kwa daraja la Primia Ligi vikiwa miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa.

Chelsea watalazimika kutoa ofa ya mlinzi wa kati Mjerumani Antonio Rudiger, 28, ya malipo ya juu zaidi kwa wiki kuliko mchezaji yeyote yule wa the Blues ili kumshawishi aongeze zaidi mkataba wake ambao unaisha mwishoni mwa msimu.
Rudiger anataka kusaini marupurupu ya zaidi ya pauni milioni 16 kwenye mkataba wake na Chelsea au asaini mkataba na Real Madrid kama wakala huru katika msimu huu.
Tetesi zinasema, Tottenham bado wanaendelea kumfwatilia mshambuliaji wa Wolves na Uhispania mwenye umri wa miaka 25 Adama Traore.

Manchester City wanajiandaa kumruhusu winga mwenye umri wa miaka 19 anayetazamiwa kufanya vyema siku zijazo Mholanzi Jayden Braaf kuondoka kwenye klabu hiyo Januari huku klabu kadhaa zikimtaka kwa mkataba wa bei nafuu huku akikaribia kumaliza mkataba wake.
Sunderland wanakaribia kukamilisha mkataba na winga wa Manchester City mwenye umri wa miaka 24 Patrick Roberts. Muingereza huyo kwa sasa anacheza kwa mkataba wa mkopo katika klabu ya Ufaransa ya Troyes.
Unaanzaje siku yako katika msimu huu wa sikukuu, mchongo upo meridianbet kasino. Sloti pendwa ya Sahara Richies inaweza kukufanya ukawa milionea katika kufunga mwaka huu, Jiunge na ufurahie kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa.

CHEZA HAPA

