Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amesisitiza kuwa klabu yake yake inarudi kwenye kufanya usajiri wa wachezaji wakubwa baada ya kumtambulisha mchezaji mpya waliomsajiri kutokea klabu ya Man city Ferran Torres.
Usajiri wa Ferran Torres umewezekana kutokana na klabu ya Barcelona kuweza kupunguza bill za mishara kwa kupunguza baadhi ya wachezaji ikiwepo kustaafu kwa Kun Aguero huku wakisubiri kupunguza tena baadhi ya wachezaji ili waweze kumuongeza kwenye kikosi Dani Alves.

Joan alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kumsajiri nyota wa timu ya Dortmund Erling Haaland japo bado wanamatatizo ya kifedha alijibu, “tunafanya kazi ya kuijenga timu, kila kitu kinawezekana ikiwa tutafanya mambo vizuri na ninauhakika tutafanikiwa, milango iko wazi kwa wachezaji wakubwa kujiunga na Barc, hakika tunairudisha hadhi yetu.”
Japokuwa Barcelona wanapitia kipindi kigumu ambapo wapo kwenye matatizo ya kifedha huku deni la likiongezeka kwa EURO1.2 bilioni mwaka jana, lakini Joan Laporta na wanachama wameweza kupitisha EURO1.5 bilioni kwa ajiri kuboresha miundombinu ya uwanja wa Camp Nou na miundombinu mingine ya klabu.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


