Hali si shwari kwenye klabu ya Liverpool kutokana na maambukizi ya COVID-19 miongoni mwa wachezaji na wafanyakazi wa klabu.
Kuelekea mchezo wa nusu fainali ya Carabao Cup dhidi ya Arsenal, Liverpool wamethibitisha maambukizi ya COVID-19 kwa kocha wao msaidizi, Pepijn Lijnders. Huu ni muongezeko wa idadi ya waathirika kwenye kikosi hicho.
Lijnders alichukua nafasi ya kuongoza timu kwenye mchezo dhidi ya Chelsea wikiendi iliyopita na, angeendelea kuwepo kwenye nafasi hiyo kwenye mchezo dhidi ya Arsenal wakati huu ambao Jurgen Klopp yupo karantini.

Kutokana na matokeo ya vipimo vya COVID-19 vilivyofanyika jana jioni, mazungumzo na waandishi wa habari pamoja na maandalizi ya mchezo dhidi ya Arsenal yaliyokuwa yamepangwa kufanywa leo, yameghairishwa.
Inaripotiwa kuwa, Liverpool wametuma barua kwa mamlaka ya EFL wakiomba mchezo dhidi ya Arsenal kughairishwa kutokana na changamoto wanayopitia.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


