Sevilla: NO Martial, NO Bakambu, TUNAFANYAJE?

Ni dhahiri kuwa, Mkurugenzi wa Michezo wa Sevilla, Monchi, yupo kwenye wakati mgumu kwenye dirisha hili la usajili. Mambo ni magumu sokoni.

Inasemekana, takribani wiki 1 imepita bila ya Monchi kuwasiliana na wakala wa Martial wala Manchester United kuhusu lengo lao la kumsajili mchezaji huyo. Hii ni baada ya United kuweka matakwa yao ambayo Sevilla wanatakiwa kuyafikia ili kumpata Martial.

Martial amebakiza miaka 3 kwenye mkataba wake na United. Kumsajili sio rahisi, United wanataka timu inayomuhitaji ilipie nusu ya mshahara wake na ada ya usajili wa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu. Hii ni ngumu kwa Monchi kwa sababu za kiuchumi.

Cedric Bakambu

“The Andalusian Club” ni kama wameachana na mpango wa Martial na wamehamishia majeshi kwa Cedric Bakambu ambaye ni mchezaji huru. Pengine kumsajili huyu inaweza kuwa rahisi. Kipengele ni, Bakambu anahitaji mshahara mkubwa na mkataba wa muda mrefu ili kujiunga na timu hiyo. Hili nalo, Monchi hawezani nalo kwa majira haya.

Kocha wa Sevilla ameweka wazi, ili timu hiyo iwezekujiweka kwenye nafasi ya kufanya vizuri msimu huu, wanahitaji kufanya usajili kwenye dirisha hili. Tofauti na hapo, lolote linaweza kutokea kuelea mwishoni mwa msimu.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.