Klabu ya Man Utd inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza iko tayari kulipa kiasi cha £67milioni ili kupata huduma ya kiungo wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic ambaye anacheza kwenye ligi kuu ya Italia Serie A klabu ya Lazio.
Chanzo maarufu cha habari nchini Itallia kilidai kuwa raisi Claudio Lotito aliyepita alitaka kumuuza Sergej Milinkovic-Savic kwa dau la 100 million euros lakini kulikuwa hakuna klbau ambayo ilikuwa tayari kulipa kiasi hicho licha tetesi kuwa man utd walifikia kiasi cha £66million.

Klabu ya Lazio wamepanga kumuuza Savic kwenye dirisha la majira ya kiangazi, ambapo hawahitajii kumpoteza bure kwani mkataba wake na klabu hiyo unaisha mwaka 2024, na wako tayari kusikiliza offa ya klabu yeyote itakayoanzia £58milion.
Klabu ya Man Utd wanahitaji saini ya kiungo huyo wa serbia mwenye miaka 27 ili kuweza kuziba nafasi ya kiungo wao Paul Pobgba ambaye anaweza kutimka kwenye klabu hiyo kwenye dirisha la usajiri wa majira ya kiangazi.
Milinkovic-Savic amecheza michezo 280 akiwa na Lazio hukua kifanikiwa kuchukua Coppa Italia mara moja na Italian Super Cup mara mbili.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


