Kocha mkuu wa klabu ya arsenal Mikel Arteta amevunja ukimya na kuthitisha kuwa hatma ya mshambuliaji wake Alexandre Lacazette kwenye kikosi chake itatuliwa baada mwishoni mwa msimu.
Mkataba wa Lacazette unakwenda kumalizika mwisho wa msimu huu na awali kulikuwa na taarifa ya kuwa mshambuliaji huyo alikaraa offer amabayo klabu hiyo ilimpatia, kwa sasa kuna taarifa kuwa Lacazette anafanyamazungumzo na klabu yake ya zamani ili aweze kurejea baada ya kuwa huru mwisho wa msimu huu.

Mikel Arteta siku ya jumapili anawakaribisha Leicester kwenye dimba la Emirates na wakati akiwa anafanya kikao na waandishi alitoa neno kuhusu hatma ya Alexandre Lacazette, “tumezungumza kwamba mwisho wa msimu, tutakapojua tupo wapi na wapi tunakwenda, kufanya maamuzi pamoja.
“Tumekubaliana kufanya maamuzi mwisho wa msimu, na lini tutafanya hivyo.”
Arteta hakutaka kwenda moja kwa moja kuwa ni wapi wanakwenda, inaweza kuwa nafasi ambayo watashika kwenye msimamo wa ligi, ndio itaamua hatama ya Lacazette.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


