Ishara mbaya ilianza baada ya kulazimisha sare mechi ya mzunguko wa kwanza wa 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid, Man United wameshindwa kutoboa kuendelea na michuano hiyo kwa kichapo cha 0-1 wakiwa nyumbani.

Renan Lodi amefanikiwa kuwasongesha mbele Atletico Madrid na kuwaachia kumbukumbu mbaya Man United ambao hawana taji kwa miaka 5 sasa.
Goli pekee, na la kwanza la Renan Lodi limewapa tiketi ya kuelekea kujitafuta kwenye robo fainali ya Ligi Ya Mabingwa. Sasa wamesalia na kibarua cha kupambana baada ya droo ijayo.
Haikuwa ishara nzuri kwa Man United kutoka sare mechi ya kwanza ya mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa. Hadi sasa, wameondolewa katika mechi nne zilizopita ambazo ishara hiyo imeonekana kwenye mechi ya ufunguzi ya mtoano, tatu kati yao zikiwa ni mechi dhidi ya wapinzani wa Uhispania.
Zaidi ya hayo, United sasa imeshinda mechi mbili pekee kati ya tisa zilizopita za Ligi ya Mabingwa wakiwa nyumbani dhidi ya wapinzani wa Uhispania.
Mastaa wa Man United walishindwa kufikia malengo ya timu, nyota kama Christiano Ronaldo akitazamwa sana kwenye mechi hii muhimu lakini akashindwa kufanya jaribio lolote golini, ikiwa ni mara ya kwanza tangia mwaka 2011 kwa mechi za Ligi ya Mabingwa alizocheza angalau dakika 45.
Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.


