LeBron James atilia shaka mustakabali wake na Los Angeles Lakers baada ya kushindwa kwao kwa kumaliza msimu na Denver Nuggets.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38, mfungaji bora katika historia ya NBA, alizua tetesi za kustaafu kufuatia kupoteza kwa 113-111 katika mchezo wa nne wa fainali za Konferensi ya Magharibi.
LeBron amesema; “Tutaona kitakachotokea mbele. Sijui nina mengi ya kufikiria, kusema ukweli. Kwangu mimi binafsi kwenda mbele na mchezo wa mpira wa vikapu, nina mengi ya kufikiria. Ulikuwa msimu wenye changamoto nyingi kwangu, kwa klabu yetu. Ilikuwa safari nzuri sana, lakini sijui.”
Nimefanya mengi na haifurahishi kwangu kutokuwa sehemu ya kufika fainali (NBA). Amesema mchezaji huyo.
James alifunga pointi 40 dhidi ya Nuggets lakini akakosa mikwaju miwili ya kufunga mchezo katika dakika za lala salama.
Hapo awali amefichua nia ya kucheza pamoja na mwanawe Bronny mwenye miaka 18, ambaye kwa sasa anacheza mpira wa kikapu chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Southern California na atahitimu NBA mwaka ujao.