Tanzania Yang’ara All African Cue Championship

Timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Pooltable imeendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi baada ya kupata ushindi katika michezo yake miwili iliyocheza jana, Februari 6, 2025.

Katika mchezo wa kwanza, Tanzania iliifunga Zimbabwe kwa fremu 14-11 kabla ya kuendeleza moto huo kwa kuwachapa wenyeji Afrika Kusini kwa ushindi mwembamba wa fremu 13-12 katika pambano lililokuwa na ushindani mkubwa hadi fremu ya mwisho.

Ushindi dhidi ya Afrika Kusini umeonekana kama kisasi kilicholipwa, kufuatia kumbukumbu ya fainali za mwaka 2023 ambapo Tanzania ilipoteza kwa fremu 11-13 dhidi ya wapinzani hao.

Tanzania Yang’ara All African Cue Championship

Kwa matokeo hayo, Tanzania sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi katika mashindano ya All African Cue Championship yaliyoandaliwa na Chama cha Pool Afrika (AAPA), yakishirikisha jumla ya timu saba.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika upande wa wachezaji binafsi (Single), Jackson Ng’anyi alimaliza safari yake ya nusu fainali baada ya kupoteza kwa fremu 3-7 dhidi ya bingwa wa Afrika Kusini, Harry Martin. Hata hivyo, bado ana nafasi ya kumaliza katika nafasi ya tatu, akitarajiwa kumenyana na Lutham Banda aliyepoteza nusu fainali dhidi ya Shaun Martheze, ambaye leo Jumamosi atachuana kwenye fainali.

Mashindano yanaendelea kwa ushindani mkubwa huku Tanzania ikiendelea kuonesha uwezo wake katika medani ya pool barani Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.