Simba leo hii atakuwa ugenini kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Atletico De Luanda kutoka kule Angola mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1:00 usiku.

Vijana hao wa Msimbazi mpaka sasa ndio vibonde wa Kundi wakiwa na pointi 1 pekee huku Petro Atletico wao wakiwa na pointi 5 walizokusanya kwenye mechi zilizopita.
Mara ya mwisho wlaipokutana katika Dimba la Benjamin Mkapa Petro Atletico waliondoka na ushindi mwembamba hivyo leo hii wakiwa nyumbani wanahitaji ushindi ili kujiweka kwenye nafasi zuri ya kufuzu hatua inayofuata.
Mpaka sasa matumaini ya Simba kufuzu ni magumu kwani kwanza kabisa inabidi ashinde mechi zake zote mbili zilizobaki huku pia akiombea mabaya kwa ambao walio juu yake akiwemo Esperence.
Kocha mkuu wa Mnyama Steve Barker akiwa ugenini leo anaamini kuwa timu yake inaweza kupata ushindi siku ya leo huku akiwa na kikosi kikubwa chenye wachezaji wenye uzoefu na michuano mikubwa.


