Arteta Aonywa Kufanya Majaribio ya Kikosi

arteta

Gwiji wa Soka na mchambuzi wa Kabumbu Gary Neville amemwambia Mikel Arteta kuacha kufanya majaribio na timu yake ya Arsenal ili kurejea kwenye njia sahihi kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Manchester United.

Washika Mtutu hao walishinda mechi zao mbili za ufunguzi wa msimu wa Premier League dhidi ya Nottingham Forest na Crystal Palace lakini walitoka sare ya 2-2 Jumamosi na Fulham.

Joao Palhinha aliipatia Fulham pointi isiyotarajiwa huko Emirates baada ya kuwalazimisha suluhu ya mabao 2-2. Mechi za EPL zina odds kubwa Meridianbet bashiri sasa.

Arteta amedai timu yake iko ‘mara 10′ kuliko msimu uliopita lakini mbinu zake kufikia sasa hazijaboresha ufasaha wao.

United wana matatizo yao wenyewe, baada ya kulazimishwa kupambana kutoka kwa mabao mawili nyuma na kuwashinda Nottingham Forest, ambao pia walimtoa nje mtu, siku ya Jumamosi. Bashiri mechi zijazo Ligi za Ulaya, Meridianbet msimu mpya mzigo wa kutosha.

Lakini Neville anaamini Arteta anahitaji tu kurudi kwenye mbinu alizozizoea msimu uliopita, wakati Arsenal ilipoisukuma sana Manchester City kwenye mbio za ubingwa.

“Nadhani wako katika hatua tofauti. Arsenal wanatarajiwa kutinga ligi kutokana na biashara waliyoifanya,’ aliambia podikasti yake ya Sky Sports.

“Wiki ijayo, ningetarajia warudi kwenye kitu ambacho kinafanana na timu iliyocheza msimu uliopita na kurejea katika misingi hiyo ya jinsi walivyo ambayo ni mfumo wa 4-3-3.”-Gary Neville.

Acha ujumbe