Azam FC Yazidi Kutanua Mbawa Zake

VIONGOZI wa Azam FC wameendeleza mwendo wa kupiga hatua zaidi kwaajili ya kuwa na wachezaji bora na kuendeleza kutoa ajira kwa Watanzania kupitia sekta ya michezo. Taarifa ambayo imetolewa na Azam FC imeeleza namna hii: “Tumeingia makubaliano ya ushirikiano na vituo vya kulea vipaji (academies) nane za mikoa mbalimbali nchini. Jisajili na Meridianbet upate bonasi kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.

 

Azam FC
Baadhi ya Wachezaji wa Klabu ya Azam FC, wakijiandaa kwa michezo yao ya Ligi Kuu ya NBC.

“Vituo hivyo nane vitakuwa ni ‘AZAM FC CENTERS’, vikituwakilisha katika mikoa husika, vikiwa na jukumu la kutafuta vipaji vya wachezaji vijana wa Kitanzania, watakaokuja kujiunga na kituo chetu ‘Azam FC Academy’ kutokana na mahitaji ya timu yetu.

“Baadhi ya vituo hivyo tulivyoanza navyo ni JK7Pro Football Center (Tanga), Tutes Hub Sports Center (Songea), Maendeleo Youth Sports Center (Mtwara), Kilwa Youth Sports Center (Lindi).

“Vingine ni Muleba Youth Sports Center (Kagera), Mwanga City Sports Center (Kigoma), Rungwe Youth Sports Center (Mbeya) na Korogwe Youth Soccer Center (Korogwe).

“Azam FC tutavipa kipaumbele vituo hivyo katika kuvuna vipaji vya vijana, pale tutakapokuwa na uhitaji wa wachezaji kwenye kituo chetu.

“Lakini sisi kama Azam FC tunaothamini vipaji vya vijana wadogo, tutaendelea na jukumu letu la kila mara la kuvuna vipaji popote pale nchini, tukiendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika juhudi zake za kukuza maendeleo ya michezo nchini.

Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.

“Tayari makubaliano kati ya vituo vyote hivyo na Azam yameingiwa kwa mikataba rasmi, zoezi lililosimamiwa kwa ukaribu na Vice Chairman, Omary Kuwe.

“Mara baada ya zoezi hilo kukamilika, hivi karibuni benchi letu la timu za vijana, litatembelea vituo hivyo (Azam FC Centers) kwa ajili ya kukutana na makocha wanaofundisha vijana hao, lengo likiwa ni kuwajenga zaidi na kuwapa vigezo vya aina ya wachezaji wanaowahitaji.

“Kwa kuanzia, tumeanza na vituo hivyo nane, lakini katika ramani yetu tumepanga kuifikia Tanzania nzima kwa kuwa na ‘Azam Centers’ katika mikoa yote nchini.

“Tunaamini kuwa kupitia programu hii, klabu yetu itaweza kuvuna vipaji bora vya vijana wa Kitanzania na kuviendeleza zaidi pale watakapofika kwenye kituo chetu ‘Azam FC Academy,”

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Acha ujumbe