Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi Ronald Koeman amejitokeza nakudai kwamba hakupewa muda na Barcelona kama muda aliyopewa Xavi huko Camp Nou.

Koeman: Xavi Amepewa Muda Mwingi Kuliko Mimi

Koeman aliletwa Barcelona Januari mwaka 2021 akichukua nafasi ya Quique Setien baada ya kipigo cha aibu cha 8-2 mwaka 2020 mwezi Agosti.

Kufuatia kuwa na matokeo duni Koeman alitimuliwa na Barca na nafasi yake ilichukulia na Xavi Hernandez ambaye alikuwa anaionoa Al-Sadd mwaka jana mwezi Oktoba.

Na baada ya muda wa ukimya tangu kuondoka kwake, kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 alizungumza na gazeti la Uholanzi la Algemeen Dagblad kutoa toleo lake la kile kilichotokea Barcelona.

Lakini anasema bado inauma sana kufikiria kurejea kwenye uwanja aliowahi kuupamba kama mchezaji.

“Hutaniona Camp Nou kwa muda, siwezi kufanya hivyo bado. Kwa rais huyu siwezi kujifanya hakuna kilichotokea,” alisema Koeman.

“Hawakunipa muda wa kutosha kama waliyompa  kocha mpya Xavi,” Koeman aliongeza bado inaniuma sababu niliwahi kupambania uwanja huu nikiwa kama mchezaji.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa