Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe aliripotiwa kuhusishwa na kutimikia Real Madrid lakini Leonardo amesema klabu hiyo itafanya kila kitu inachoweza kumfanya nyota huyo kusalia klabuni hapo.

Katika mahojiano ya kina na L’Equipe, Leonardo alitoa ufafanuzi katika masuala yote. Hakumuongelea Mbappe pekee, bali pia alizungumzia kuhusu Lionel Messi, usajili wa Sergio Ramos na mustakabali wa kocha Mauricio Pochettino.

Leonardo alithibitisha kuwa bado hakuna ofa yoyote iliyotumwa kwa Mbappe, kufuatia ripoti za ofa ya kandarasi yenye thamani ya euro milioni moja kwa wiki.

“Hatujatuma ofa maalum. Kuna kipengele muhimu: Nadhani kitu cha mwisho ambacho tutaweka katika mkataba huu ni pesa. Tunataka kumweka katika mazingira bora zaidi ili kumfanya kuwa mchezaji bora zaidi.

“Hatujawahi kuzungumza juu ya pesa. Kwa sababu sio juu ya hilo. Kylian ana thamani kubwa sana ambayo nadhani hiyo ni ya pili. Nadhani kuweka kiasi hicho, itachukua dakika mbili.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa