Mlinzi wa Barcelona Jean-Clair Todibo amejiunga na klabu ya Ligue 1 Nice kwa dili ya mkopo mpaka mwisho wa msimu huu.

Todibo Asaini Nice kwa Mkopo Akitokea Barca.

Klabu hiyo ya Ligue 1 katika makubaliano yao kuna kipengele kitakacho waruhusu kumnunua moja kwa moja kwa dau la €8.5m mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

Todibo aliiunga na Barcelona miaka miwili iliyopita akitokea klabu ya Toulouse na alikuwa akitajwa kama moja ya wachezaji makinda wenye kipaji katika soka la Ulaya.

Hakufanikiwa kufunga goli lolote katika Michezo yake miwili ya LaLiga katika timu Barcelona msimu wa 2018-19 walipocheza dhidi ya Huesca ikifutiwa na mchezo walipoteza kwa 2-0 dhidi ya Celta Vigo.

Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Todibo kuhama katika dirisha la mwezi Januari baada ya kujiunga na Schalke kwa mkopo mwaka uliyopita na kufanikiwa kucheza michezo nane ya Bundesliga lakini dili ya kumnunua moja kwa moja kwa kitita cha €25m ilibuma.

Fursa yake ya kuendelea kuwa na The Blaugranas msimu huu ili kumbwa baada ya kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona mwezi Agosti baada ya kufanyiwa vipimo.


TUNGENEZA FAIDA KUPITIA KASINO YA MERIDIANBET

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa