F1 2021: Ni Makosa Ya Kibinadamu

Ni dhahiri, ubingwa wa Formula 1 (F1) mwaka 2021 bado ni gumzo miongoni mwa mashabiki wa mchezo huo. Haki ilitendeka au iliminywa mahali?

Mvutano mkali wa maamuzi ya mchezo huo ulitokea kwenye mbio za Abu Dhabi GP ambapo, hizi ndio zilikua mbio za kumaliza msimu wa 2021. Hata hivyo, 2021 ulikuwa ni mwaka wa kipekee kwenye F1 kutokana na upinzani mkali uliokuepo kati ya Lewis Hamilton (Mercedes) na Max Verstappen (Red Bull).

Hamilton (kushoto) akiwa na Verstappen (kulia)

Yote kwa yote, Verstappen aliibuka kinara wa mbio zile na, akatangazwa kama bingwa wa Formula 1 kwa mwaka 2021 ikiwa ni mara yake ya kwanza kutwaa taji hilo kubwa duniani (kwenye mchezo wa mbio za langalanga).

Muda mfupi baada ya mbio za Abu Dhabi GP kutamatika, timu ya Mercedes ilieleza malalamiko yake kwa usimamizi wa mbio hizo kwa kile walichodai ni kushindwa kufuata sheria sahihi za uamuzi. Hii iliibua hisia za mashabiki na hasa uongozi wa timu ya Mercedes. FIA ilisimamia msimamo wake na kuahidi kulifanyia uchunguzi sakata hilo.

Hatimaye, matokeo ya uchunguzi wa FIA yamewekwa wazi. Kwa ilivyoonekana, mwamuzi wa mbio zile alifanya makosa ya kibinadamu ambayo kwa namna moja ama nyingine, yaliathiri mchezo husika. Hata hivyo, ubingwa wa Max Verstappen hautaathirika na matokeo ya uchanguzi huo na hivyo, maamuzi yaliyofikiwa ni sahihi na halali.


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe