Harvey Elliott anatarajia kufanyiwa upasuaji leo jijini London baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu katika mechi dhidi Leeds United.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18 alipata majeraha hayo baada ya kugongana na Pascal Struijk katika mechi iliyoisha kwa liverpool kupata ushindi wa goli 3-0.

“Niliongea na Harvey Elliott usiku wa jana, hakuwa katika hali nzuri na amekubaliana na hali kuwa atakuwa nje kwa muda.” alisema Klopp kwenye kikao na waandishi wa habari.
“Sasa hivi yuko London, kwa taarifa nilizonazo nadhani anaweza kuwa tayari kashafanyiwa upasuaji.”Tunasubili habari kutoka kwao baada ya upasuaji.
Liverpool wanajiandaa kuwakaribisha miamba ya Serie A Ac Milan katika ligi ya mabingwa, mchezo huo utapigwa katika dimba la Anfield siku ya jumatano.
Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii.!


