Benard Morrison - Naishukuru Yanga kwa Kunipa Nafasi

Baada ya kuibuka mshindi kwenye kesi dhidi ya timu yake ya zamani Yanga Africans mtukutu Benard Morrison ameamua kutoa shukrani kwa uongozi,wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwakumpokea na kumuunga mkono wakati wote alipokuwa akiitumikia timu hiyo.
Benard Morisson
Benard Morisson
Kupitia ukurasa wake rasmi kwenye mtandano wa Instagram Morrison amesema anatambua nafasi aliyowahi kuipata kuitumikia timu hiyo huku akimtaja kocha Luc Aymael kuwa ndiye mtu pekee alietambua uwezo wake na kumleta Yanga.

Kuhusu kocha Luc mchezaji huyo ametumia mfano wa daktari kwakusema “Daktari mbaya aliyemhudumia mgongwa wakati daktari mzuri anasubiriwa kuja mchango wake unapaswa kuheshimiwa” na huo ni msemo ambao amesema unatumiwa sana kwao nchini GHANA.

Morrison hajaishia hapo kuhusu mfano wa Daktari ameongeza kuwa “Pamoja na ubaya wa Daktari lakini ndiye alifanya uhai wa mgonjwa kuendelea kuwepo hadi alipokuja daktari mzuri”

Ni wazi Morrison anawakumbusha wananchi kuwa pamoja na kumtimua kocha huyo aliemleta Bongo wanapaswa kumheshimu na kutambua mchango wake kwa mambingwa hao mara ngingi wa ligi kuu bara.

Benard Morisson
Benard Morisson

Mwisho Benard Morrison amesema hizi ni shukrani zake rasmi kwa Yanga na wote waliomfanya afurahi akiwa anaihudumia timu hiyo ambayo haijapoteza mechi yeyote ya ligi tangu kuanza msimu huu wa ligi kuu 2021/22.

Amemaliza wakili msomi Benard Morrison kwakusema hajawasahau mashabiki wa Yanga kwa upendo wao kwake alipokuwa Jangwani.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.