Jaribu kufikiria ligi ya mabingwa ulaya itakuwaje bila Juventus msimu ujao, hakuna Ronaldo, Dybala, wala Buffon ndani ya UEFA Champions League! Itakuwa kitu cha kushangaza na kupoteza ladha sana!

Mabingwa hao wa kihistoria wa Turin walikubali kipigo cha 3-0 kutoka kwa AC Milan wakiwa nyumbani kabisa! Mechi hii ilikuwa ni moja ya mechi muhimu sana kwa Juventus lakini mambo hayakuwa sawa upande wao!

Magoli ya  Brahim Diaz, Ante Rebic na Fikayo Tomori yalitosha kuwapa ushindi huo mnono timu ya Ac Milan ambao umewafanya wapande mpaka nafasi ya tatu wakiwa na alama 72. Juventus wamebakiwa na michezo miwili tu ili kutambua hatima yao kwenye UEFA msimu ujao.

Mabingwa hawa wa kihistoria wa Turin walipoteza ubingwa walioshika kwa misimu tisa mfulululizo mbele ya Inter Milan juma lililopita, na sasa wanaweza poteza nafasi ya kucheza UEFA msimu ujao.

Mechi ya mwisho ya Juventus itakuwa dhidi ya mabingwa wapya Inter Milan tarehe 15 mwezi wa tano. Je, itakuwa ni mwisho wa utawala wa timu hiyo kwenye kurasa za michezo duniani?

PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Juventus, Ipi Hatima Ya Juventus UCL Baada Ya Kupigwa 3-0?, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa