Siku ya jumatatu, Barcelona ilitangaza Sergio Aguero kama mchezaji wao kwa miaka miwili baada ya kuhama City, kwa upande wa pili Kane ametajwa kuwa mrithi wa pengo la Aguero pale Etihad.

Aguero ameacha historia kubwa Man City, 260 ndio namba ya magoli aliyofunga, namba inayomfanya yeye mfungaji bora wa muda wote wa Manchester City na wanne katika wafungaji bora wa muda wote wa Premier League.

Kane

City ina majukumu ya kutafuta mrithi wa Aguero licha ya ukweli kuwa hawawezi kupata mtu atakayefanya kazi hiyo kama alivyofanya muajentina huyo. Habari kutoka Skysports zinadai kuwa mwenyekiti wa City Khaldoon Al Mubarak amethibitisha watafuta straika majira haya ya joto.

Mabingwa hao wa EPL wanaweza kupata saini ya majina kadhaa yakiwemo, Romelo Lukaku, Erlinga Haaland na Harry kane. Inter Milan wameona umuhimu wa Lukaku hivyo uwezekano wa yeye kuendelea kusalia Serie A ni mkubwa zaidi.

Kwa upande wa Erling Haaaland, kulikuwa na tetesi nyingi kuwa mchezaji huyu angetua City lakini, ripoti nyingi hivi sasa zinadai kuwa mchezaji huyu atatua hispania.

Kane

Kitu ambacho kinamuacha Kane kama salio pekeee, ambaye ni mfungaji bora wa EPL msimu wa 2020/2021. Katika moja ya mahojiano yake, Kane alidai kuwa anatamani kupata changamoto sehemu nyingine na anataka kwenda kucheza na timu itakayoshiriki michuano mikubwa.

Kingine, Harry alidai kuwa anatamani sana kwenda kucheza na Kevin De Bruyne ambaye anajua sana kutoa pasi nzuri za magoli.


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

ONI MOJA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa