Mshambuliaji wa AS Roma, Paulo Dybala, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki sita baada ya kupata jeraha la goti, hali inayoweza kuathiri harakati za timu hiyo katika mbio za kufuzu UEFA Champions League kupitia Serie A.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Italia, La Gazzetta dello Sport na Sky Sport Italia, Dybala alifanyiwa upasuaji mjini Roma Ijumaa baada ya kubainika kuwa na mpasuko kamili wa meniscus ya nje kwenye goti lake.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Awali mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alilazimika kusitisha mazoezi ya timu siku ya Alhamisi baada ya kuhisi maumivu ambayo klabu ilieleza kuwa ni uchovu wa misuli. Hata hivyo uchunguzi wa baadaye ulithibitisha jeraha kubwa zaidi lililohitaji kufanyiwa upasuaji.


Dybala hakucheza mechi yoyote ya Roma mwezi Februari kutokana na kile kilichoelezwa kuwa tatizo la goti. Alirejea kwenye benchi katika mchezo dhidi ya Juventus FC Machi 1, lakini hakupata nafasi ya kucheza katika sare ya mabao 3-3.
Msimu huu Dybala amefunga mabao mawili pekee katika mechi 17 za Serie A. Kwa sasa Roma inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa nyuma kwa pointi 16 dhidi ya vinara Inter Milan, huku ikiwa pointi mbili nyuma ya SSC Napoli walio nafasi ya tatu na pointi tatu mbele ya Como 1907 walio nafasi ya tano.


