Klabu Ina Matatizo, Sio Mimi - Mourinho

Jose Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham Spurs amesema kuwa anadhani timu hiyo ina matatizo na kusifu mbinu zake kuwa ni bora.

Kwa sasa amekuwa kwenye mwendo wa kususua tofauti na awali jambo ambalo linaweka hatari kibarua chake baada ya kurithi mikoba ya Mauricio Pochettino ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha PSG.

Februari 21 alishuhudia timu yake ikipoteza mbele ya West Ham United kwa kufungwa mabao 2-1 jambo ambalo limemfanya awe mnyonge kwa kiasi chake.

Kinakuwa ni kichapo cha tano ndani ya Ligi Kuu England kati ya mechi sita ambazo ameongoza kikosi chake ambapo kwenye mchezo huo alishuhudhia mabao ya Michail Antonio na Jesse Lingard na kwa Spurs ilifunga bao lake kupitia kwa Lucas Moura.

Mourinho amesema:”Klabu ina matatizo na siwezi kuyatatua peke yangu,tunapoteza mechi nyingi haya ni matokeo mabaya. Kuhusu mbinu sisi na benchi la ufundi tuna mbinu bora kabisa,“.

Spurs imecheza jumla ya mechi 23 kibindoni imekusanya jumla ya pointi 24 ipo nafasi ya 9.


TENGENEZA FAIDA KATIKA SLOTI PENDWA HAPA MERIDIANBET

BusttheBank ni sloti inayokupa Mkwanja wa kutosha. Ndio, hii ni sloti inayokupa faida ya hadi mara kibao ya dau lako. Ni Meridianbettz pekee utakapoweza kupata burudani hii.

CHEZA HAPA

8 Komentara

    Kweli muorinho kweli umeongea sahihi

    Jibu

    Mmeshuka kiwango

    Jibu

    Anachosema Mourinho ni sahihii

    Jibu

    Asante kwa taalifa

    Jibu

    M nakuelewa sana baba

    Jibu

    Mourinho Yuko sahihi

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Mzee wa kujitoa

    Jibu

Acha ujumbe