Hatima ya ubingwa wa Ligue 1 ilitegemea mechi za mwisho kuamua nani atainua kombe hilo. Vita kubwa ilikuwa ni kati ya Lille na PSG ambao walitegemewa sana kufanikisha mbio hizo na kubeba taji.
Lille walikuwa ugenini kucheza na Angers na ushindi wa 2-1 ulikuwa muhimu sana kuhakikisha kuwa wanatangazwa mabingwa wa ligi hiyo. Kwa upande wa pili, PSG walihitaji ushindi na karoho cha ubaya kwa Lille wapoteze.
PSG walikuwa ugenini wakicheza na Brest ambapo goli la kujifunga la Romain Faivre na lile la Kylian Mbappe yalitosha kabisa kuwapa ushindi wa 2-0 PSG lakini haukutosha kuwapa taji la Ligue 1. Katika mechi hiyo pia Neymar alikosa penati.
Lille wanashinda taji la Ligue 1 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, toka wafanye hivyo mwaka 2011. Baada ya ushindi na kutangazwa mabingwa hapo jana, mashabiki na wadau mbalimbali wa Lille walitoa pongezi zao.
“Ubingwa huu ni mkubwa sana. Imekuwa ni muda mrefu na kumekuwa na presha kubwa. Kuishinda PSG kwenye mbio za ubingwa, wachezaji walikuwa wazuri sana. walikuwa mashujaa“, alisema Galtier kwa jarida la Canal+.
BONASI YA 50% KILA SIKU KATIKA KASINO ZA EVOPLAY HAPA MERIDIANBET.
Meridianbet na Evoplay Kasino wanakupa bonasi ya 50% ya kiasi utakachoweka katika akaunti yako leo. Unasubiri nini ni wakati wa kupiga pesa sasa na Mabingwa.