Beki Mfaransa Lucas Hernandez alikua mmoja wa walinzi ghali zaidi katika historia alipokuwa akiagana na klabu yake ya zamani Atletico Madrid na kwenda Bayern Munich mwaka 2019 kwa dau la  €80m. 

Hernandez anadaiwa kuwa kwa sasa yupo tayari kurejea Atletico, bila kujali kushuka kwa gharama ya uhamisho wake.

Herandez

Hernandez kwa sasa ni majeruhi baada ya kupata changamoto kwenye gemu dhidi ya Barcelona mwezi Septemba lakini amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Bavaria katika miaka ya hivi karibuni.

Hernandez ataikosa mechi ya marudiano Jumatano jioni kutokana na jeraha hilo, ingawa Bayern Munich tayari wamethibitishwa kumaliza kama vinara wa kundi lao la Ligi ya Mabingwa.

Akiongea na Partidazo Cope, Hernandez alithibitisha kwamba ikiwa fursa hiyo itajitokeza, atachukua nafasi hiyo.

“Ikiwa siku moja chaguo la kurejea Atletico litatokea, kwa nini nisirejee? Ningependa itokee. Litakuwa jambo zuri.”

 

Atletico Madrid ndiyo klabu iliyonipa kila kitu. Mimi ni zao la akademi na nimekuwa nikiipenda timu kila wakati. Tangu nilipoondoka nimewatakia kila la kheri”.

Lucas Hernandez

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa