Mtangazaji wa Ghana Benjamin Wille Graham amechaguliwa na FIFA kutangaza matukio yatakayokuwa yanaetokea na kuendelea kwenye michezo ya kombe la dunia inayotarajia kuanza mwezi novemba 21 nchini Qatar.
Mtangazaji huyo wa kimataifa kutoka nchini Ghana, kwa sasa anafanya kazi kama meneja masoko kwenye sherikisho la mpira nchini humo, Graham anatarajiwa kufanya kazi na FIFA kwa kutoa matangazo ambayo yatawaburudisha watazamaji kwa kuzitaja timu, ikihusisha kutangaza ndani ya uwanja, kuwa MC na sambamba kumuongoza DJ ili kutengeneza hali ya hewa ya kuvutia ndani ya Uwanja.
Hii ni mara ya kwanza kwa FIFA kumchagua Mtangazaji ambaye atazitambulisha timu kwenye kombe la dunia kutokea nchini Ghana.
Graham ameshawai kufanya kazi kwenye vyombo vya habari kama, SuperSport, Startimes, Foxsports Africa, ESPN lagardele na CAF kama kingozi wa mtangazi wa mpira kwenye ligi ya Ghana Premier League, Africa Cup of Nation na michuano ya kufuzu kombe la dunia, pia alishawai kutangaza CHAN, WAFU nakadhalika.
Graham pia alishawai kufanya kazi kama mtangazaji wa msimu na watangazaji kama Barry Lambert, Paul Dempsey, Steve Vickers, Robbie Knox na Duane D’llprcaor.
Graham ana master’s degree kwenye Media Management kutoka Ghana Institute of Journalism.