Kitendo cha Yanga kuamua kuwahi mapema uwanjani kisha kuondoka bila kusubiri muda mpya uliotangazwa kwa ajili ya mchezo huo, umepongezwa na staa wa zamani wa Yanga na Simba akisema ni sahihi kulingana na sheria za soka.

malima, Malima Aipa Tano Yanga, Meridianbet

Beki wa zamani wa Kimataifa wa Yanga, Simba na Taifa Stars, Bakari Malima amesema kuwa mtu aliyetoa Amri ya kusogeza mechi mbele kutoka saa 11:00 jioni hadi 1:00 usiku anatakiwa kuwajibishwa kwani ni ishara ya kuwagawa Watanzania katika makundi mawili.

Malima amesisitiza kuwa Yanga wamezingatia kanuni na sheria ya michezo inavyotaka, hivyo kitendo cha TFF kuahirisha ikitoa sababu ya kupokea maelekezo ya Wizara bila maelekezo yaliyoshiba sio tu cha kiungwana, lakini pia inaonyesha jinsi gani soka la Tanzania lina safari ndefu ya kufika.

malima, Malima Aipa Tano Yanga, Meridianbet

“Wanataka kumpa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu majaribu, angekuwa hayati John Magufuli yupo hai angeshatoa tamko kabla ya Yanga kuondoka uwanjani.” alisema Malima na kuongeza:

“Aliyesababisha hayo anatakiwa achukuliwe hatua na aseme sababu ilikuwa ni nini hadi asogeze muda huo kiholela wakati anatambua upinzani mkali baina ya timu hizo.” (Malima via Mwananchi)


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

malima, Malima Aipa Tano Yanga, Meridianbet

SOMA ZAIDI

12 MAONI

  1. Kila mtu anakosa kwasababu kila mtu alifika uwanjani nalefa akuingia uwanjani kilicho baki walaumiwe ngazi zajuu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa