Aston Villa wanabaki bila nahodha Jack Grealish kwa mechi ya 12 mfululizo, lakini anaweza kurudi kucheza na Everton siku ya Alhamisi.
Uchambuzi EPL: Aston Villa vs Manchester United
Aston Villa vs Manchester United

Kiungo Morgan Sanson pia bado yupo nje na jeraha la goti.

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer aliripoti kuwa hana tatizo la majeruhi kufuatia mchezo wao wa Europa League dhidi ya Roma.

Lakini, kutokana na kwamba wanacheza mara nne kwa siku nane tu, atakizungusha kikosi chake.

Rekodi za Kukutana 

Manchester United hawajafungwa katika mechi 21 za mwisho za EPL ugenini dhidi ya Aston Villa tangu walipoteza 3-1 siku ya ufunguzi wa kampeni ya 1995-96.

Ole Gunnar Solskjaer alikuwa katika timu ya mwisho ya Manchester United kupoteza mchezo huko Villa Park wakati walichapwa 3-0 katika pambano la Kombe la Ligi raundi ya tatu mwaka 1999.

Aston Villa wamepata ushindi mmoja tu katika mikutano 44 ya Premier League na hawajashinda katika michezo 16 yao ya mwisho dhidi ya United tangu ushindi wa 1-0 huko Old Trafford mwezi Desemba 2009.

Villa imepoteza mechi tisa za Ligi Kuu mwaka 2021 – ni pande tatu tu ndizo zimekuwa mbaya zaidi. Villans walipoteza mechi nne tu kati ya 14 za ligi msimu huu kabla ya mwaka kuanza.

Wanalenga kushinda michezo mfululizo ya ligi kwa mara ya kwanza tangu Desemba.

Ni Chelsea na Manchester City tu ndio wameweka clean sheet nyingi zaidi za EPL msimu huu kuliko zile 14 za Villa, lakini, hakuna timu inayoongoza kwa kukimbia kwa mechi nyingi bila clean sheet kama saba ya Villa.

Manchester United hawajafungwa katika mechi 24 za ugenini za Ligi Kuu (W15, D9), ikiwa ni pungufu tatu ya rekodi kubwa ya Arsenal iliyowekwa kati ya Aprili 2003 na Septemba 2004.

Manchester United imepoteza mchezo mmoja tu kati ya 27 ya Premier League msimu huu (W17, D9).


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

Aston Villa, Uchambuzi EPL: Aston Villa vs Manchester United, Meridianbet

SOMA ZAIDI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa