Klabu ya Manchester United inahitajika na matajiri wa kiarabu kutoka nchini Qatar huku mabosi hao wakiwasilisha ofa yao siku ya jana kwajili ya kuinunua klabu hiyo iliyopo sokoni kwasasa.
Miezi kadhaa iliyopita klabu ya Manchester United iliwekwa sokoni na waliokua wamiliki wa muda mrefu klabuni hapo maarufu kama famili ya Glazers, Huku matajiri mbalimbali wakihitaji kuinunua klabu hiyo yenye historia kubwa katika soka la Uingereza na dunia kwa ujumla.
Mapema jana mwenyekiti wa benki ya kiislamu huko nchini Qatar Sheikh Jasim bin Hamad bin Al Thani aliwasilisha ofa ya kuinunua klabu ya Manchester United, Huku akiweka baadhi ya vipaumbele vyake na moja wapo ni kurudisha hadi ya klabu hiyo ndani na nje ya uwanja na vilevile kurudisha mioyo ya mashabiki wa klabu hiyo iliopoteza imani na klabu hiyo.
Sheikh Jasim bin Hamad bin Al Thani katika taarifa yake aambayo aliwasilisha maombi ya kuinunua klabu hiyo pia alisema anataka kuwekeza kwenye mpira, kituo cha mazoezi, uwanja na miondombinu mingine kwa upana zaidi ikiwa ni katika lengo lilelile la kuirudishia heshima klabu hiyo ambayo inaonekana kama imepotea kwasasa.
Mashabiki wa klabu ya Manchester United wengi wao wameonekana kufurahishwa na taarifa matajiri kutoka nchini Qatar kutaka kuinunua klabu ya Manchester United, Kwani wanaamini ndio mwanzo wa klabu yao pendwa kurejea katika zama zake za ushindi baada ya kupitia kipindi kigumu kwa muda mrefu.

