Kylian Mbappe anaripotiwa kuwa kwenye hati hati ya kuikosa gemu ya Paris Saint-Germain katika mechi ya Mzunguko wa pili 16 bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu Jumatano baada ya kupata jeraha kwenye mazoezi leo. Atafanyiwa majaribio zaidi katika saa 48 zijazo.
Habari hizo ni pigo kubwa kwa PSG kutokana na jinsi Mfaransa huyo alivyo muhimu kwao. Bao lake la dakika za lala salama katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Parc des Princes ndiyo liliamua mchezo mkali na kutokuwepo kwake kungeweza kuwapa nafasi Madrid.

Los Blancos pia wanakosa wachezaji kadhaa muhimu. Ferland Mendy na Casemiro wote wamesimamishwa huku kukiwa na shaka juu ya Toni Kroos na Fede Valverde kutokana na majeraha na ugonjwa.
Madrid wako kileleni mwa La Liga, wakiwa na pointi nane zaidi ya Sevilla wanaoshika nafasi ya pili. Waliichapa Real Sociedad 4-1 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu Jumamosi jioni. PSG pia wako kileleni mwa Ligue 1 kwa pointi 13 lakini walifungwa 1-0 na Nice Jumamosi usiku.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


