Mechi ya kirafiki kati ya Hispania na Misri yafutwa ghafla

Mechi ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya Hispania na timu ya taifa Misri iliyokuwa ipigwe mwezi huu imefutwa kutokana na sababu za kiutawala, kwa mujibu wa vyanzo viwili vilivyo karibu na Shirikisho la Soka la Misri na timu ya taifa.

Mechi ya kirafiki kati ya Hispania na Misri yafutwa ghaflaMchezo huo ulikuwa umepangwa kuchezwa Machi 31 nchini Qatar kama sehemu ya maandalizi ya FIFA World Cup, lakini hali ya usalama katika ukanda wa Ghuba imeathiri mipango hiyo kufuatia mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Ripoti za vyombo vya habari vya Misri zilieleza uwezekano wa kuhamishia mchezo huo nchini Hispania, lakini mpango huo pia ulishindikana kutokana na changamoto mbalimbali za maandalizi.

Chanzo kimoja kilisema: “Baadhi ya wachezaji wa Misri hawakuwa na visa za kuingia Ulaya au Hispania, na hakukuwa na muda wa kuomba kutokana na sikukuu zilizokuwa zinakaribia.”

Mechi ya kirafiki kati ya Hispania na Misri yafutwa ghaflaChanzo kingine kiliongeza: “Mashirikisho yote mawili hayakufikia makubaliano juu ya baadhi ya masuala ya msingi. Awali Qatar iligharamia kila kitu, lakini safari hii hali ilikuwa tofauti.”

Baada ya kufutwa kwa mchezo huo, Misri sasa itacheza na timu ya taifa ya Saudi Arabia jijini Jeddah Machi 27, huku Hispania wakitarajiwa kucheza dhidi ya timu yataifa ya Serbia siku hiyo hiyo. Misri imepangwa Kundi G pamoja na timu ya taifa ya Belgium,timu ya taifa ya New Zealand na timu ya taifa ya Iran, wakati Hispania wakiwa Kundi H na timu ya taifa ya Cape Verde, Saudi Arabia na Uruguay.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.