Ronaldo Asafiri Kwenda Hispania Kwa Matibabu ya jeraha la Paja

Mshambuliaji wa Al Nassr na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo, anatarajiwa kusafiri kwenda Hispania kwa ajili ya matibabu baada ya kupata jeraha la msuli wa paja. Kocha wa Al Nassr, Jorge Jesus, alithibitisha taarifa hiyo Ijumaa akieleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya madaktari wa timu kufanya uchunguzi wa kina kuhusu hali ya mchezaji huyo.

Ronaldo Asafiri Kwenda Hispania Kwa Matibabu ya jeraha la Paja

Ronaldo mwenye umri wa miaka 41 alipata jeraha hilo mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Saudi Arabia ambapo Al Nassr iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Al Fayha.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Ronaldo Asafiri Kwenda Hispania Kwa Matibabu ya jeraha la Paja

Kocha Jesus alisema baada ya uchunguzi kubainika kuwa Ronaldo anahitaji muda wa kupumzika pamoja na matibabu maalum, hivyo timu imeamua kumpeleka Hispania kwa ajili ya kuendelea na programu ya kupona. Kutokana na jeraha hilo, Ronaldo hatashiriki katika mchezo ujao wa Al Nassr pamoja na mechi inayofuata dhidi ya Al Khaleej katika mashindano ya Saudi Pro League.

Hata hivyo, bado haijafahamika kama mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or mara tano atakuwa fiti kushiriki mechi za kirafiki za kimataifa ambapo Ureno itacheza dhidi ya Mexico national football team Machi 29 na United States men’s national soccer team Aprili 1.

Ronaldo Asafiri Kwenda Hispania Kwa Matibabu ya jeraha la Paja

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.