MO Dewji Awasilisha Rasmi Mpango wa Uwanja Mpya wa Simba

Mwekezaji na Rais wa heshima wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji, amechukua hatua muhimu kuelekea maendeleo ya klabu hiyo baada ya kuwasilisha rasmi barua ya ujenzi wa uwanja mpya kwa Bodi ya Wadhamini wa Simba.

MO Dewji Awasilisha Rasmi Mpango wa Uwanja Mpya wa SimbaHatua hiyo inakuja kufuatia kukamilika kwa mchoro wa mradi huo mkubwa unaojulikana kama The Great Simba Project.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo vya ndani, bilionea huyo tayari amewasilisha nyaraka zote muhimu kwa Bodi ya Wadhamini akilenga kupata idhini ya kuanza utekelezaji wa mradi huo bila kuchelewa. Uwasilishaji huo unaonekana kuwa mwanzo wa mageuzi makubwa ya miundombinu ndani ya klabu hiyo kongwe nchini.

 

Mradi huo unapendekezwa kutekelezwa katika eneo la Bunju, jijini Dar es Salaam, ambapo ardhi inayofaa tayari imeainishwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo ya kisasa. Eneo hilo linatajwa kuwa na sifa zote zinazohitajika kwa ujenzi wa uwanja wa kisasa wenye hadhi ya kimataifa.

MO Dewji Awasilisha Rasmi Mpango wa Uwanja Mpya wa SimbaMbali na uwanja wa mpira wa miguu, mradi huo pia utahusisha ujenzi wa viwanja vya mazoezi vya kisasa vitakavyotumika na timu zote za Simba. Hii ni pamoja na kuboresha mazingira ya mafunzo kwa wachezaji ili kuongeza ushindani na ubora wa timu.

Aidha, mpango huo unajumuisha ujenzi wa hosteli za kisasa kwa ajili ya timu ya wakubwa (Senior Team), timu ya wanawake pamoja na timu za vijana. Lengo ni kuhakikisha kuwa wachezaji wanapata mazingira bora ya kuishi na kufanya maandalizi yao kwa ufanisi zaidi.

MO Dewji Awasilisha Rasmi Mpango wa Uwanja Mpya wa SimbaUtekelezaji wa The Great Simba Project unatarajiwa kuanza mara moja baada ya Bodi ya Wadhamini kutoa idhini rasmi. Endapo mradi huo utakubaliwa, utakuwa hatua kubwa katika kuifanya Simba kuwa na miundombinu ya kisasa itakayoiwezesha kushindana katika viwango vya juu zaidi ndani na nje ya nchi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.