Kocha wa timu ya taifa ya Italia, Gennaro Gattuso, ameomba radhi kwa mashabiki na taifa kwa ujumla baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu kucheza FIFA World Cup kwa mara ya tatu mfululizo.
Italia ilitolewa katika hatua ya mtoano baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Bosnia and Herzegovina katika mchezo uliopigwa Zenica.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Italia, mabingwa wa dunia mara nne na waliotwaa taji hilo mwaka 2006, walipata bao la kuongoza mapema kabla ya kupoteza mchezaji mmoja na kubaki 10 uwanjani. Hali hiyo iliwapa nafasi wapinzani kusawazisha na hatimaye mchezo kwenda hadi mikwaju ya penalti iliyowaondoa Italia.
Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Italia kushindwa kufuzu Kombe la Dunia, jambo linaloendelea kuwa pigo kubwa kwa soka la nchi hiyo. Licha ya kuonyesha kiwango kizuri katika baadhi ya vipindi vya mchezo, matokeo hayo yameacha maumivu makubwa kwa mashabiki na wadau wa soka nchini humo.
Kocha Gattuso, ambaye alichukua nafasi ya Luciano Spalletti mapema kwenye kampeni ya kufuzu, alikataa kuzungumzia mustakabali wake baada ya mchezo, akisisitiza kuwa lengo kuu lilikuwa kufuzu Kombe la Dunia.
“Tulistahili matokeo bora zaidi leo. Tulibaki na wachezaji 10 lakini bado tulipata nafasi kadhaa nzuri. Naomba radhi, huu ni mchezo wa soka na nina fahari na wachezaji wangu,” alisema Gattuso kwa hisia kali.
“Mustakabali wangu si muhimu kwa sasa, muhimu ilikuwa kufuzu Kombe la Dunia. Inaumiza sana, ni pigo gumu kulikubali. Tulihitaji ushindi huu kwa ajili yetu na kwa Italia nzima,” aliongeza Gattuso. Mkuu wa Shirikisho la Soka Italia (FIGC), Gabriele Gravina, amesema anamtaka Gattuso aendelee kubaki kuinoa timu hiyo licha ya presha kubwa iliyopo.

