Kocha mpya wa Manchester United, Ralf Rangnick huenda akaanza kibarua chake cha kuinoa timu hiyo Alhamis hii watakaposhuka dimbani kupepetana na Arsenal.
Mjerumani huyo amethibitishwa mapema jana kuwa kocha wa muda wa kikosi cha mashetani hao wekundu kwa mkataba wa hadi mwezi Juni mwakani huku akiwa na kipengere cha kuhudumu katika nafasi za uongozi ndani ya klabu hiyo kwa miaka miwili baada ya mkataba wake wa kocha wa mpito kukamilika.
Rangnick ni kati ya walimu wenye heshima kubwa nchini Ujerumani akisifika kwa utashi wake wa mbinu wa soka la kushambulia pamoja na muunganiko wa timu.
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.